HabariNewsSiasa

Kizaaza kinatarajiwa kushuhudiwa wakati wa mkutano wa Naibu wa Rais William Ruto katika Kaunti ya Bomet.

Kizaaza kinatarajiwa kushuhudiwa wakati wa mkutano wa Naibu wa Rais William Ruto katika Kaunti ya Bomet hii leo baada ya viongozi wanaowania ugavana katika Kaunti hiyo kutofautiana vikali kuhusu ni nani hasa anayefaa kuhudhuria.
Makundi ya wafuasi wa Gavana Hillary Barchok na wale wa aliyekuwa Gavana wa Kaunti hiyo Issac Ruto walikabiliana vikali wakati wa kuandaa ukumbi wa hafla hiyo.
Issac Ruto ambaye pia ni mwendani wa Naibu wa Rais ambaye ana azma ya kuwania ugavana wa Kaunti hiyo dhidi ya Gavana Barchok, amekosoa msimamo wa Barchok akisema kwamba kila kiongozi anaruhusiwa kuhudhuriwa.