HabariNewsSiasa

SENETA WA MERU MITHIKA LINTURI KUFIKISHWA MAHAKAMANI HII LEO.

Seneta wa meru Mithika Linturi anatarajiwa kufikishwa Mahakamani hii leo ili kufunguliwa mashtaka ya madai ya kutoa matamshi yenye uchochezi.
Seneta Linturi amekesha korokoroni usiku kucha baada ya kukamatwa makachero wa idara ya upelelezi DCI katika afisi ya tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC hapo jana akiwa mjini Eldoret kisha usafirishwa hadi Nairobi ili kuhojiwa.
Anapofikishwa Mahakamani hii leo, Maafisa wa Uchunguzi wanatarajiwa kuomba Mahakama kuagiza kuzuiliwa kwa Linturi kwa siku kadhaa ili kukamilisha uchunguzi.
Wakili wa Linturi Alias Mutuma amesema kukamatwa kwa Linturi, kumechochewa kisiasa na kwamba Serikali inalenga kumzuia kushiriki katika mijadala ya mswada wa marekebisho ya sheria za Vyama vya Kisiasa hapo kesho ndani ya Bunge la Seneti.
Wakili Mutuma amesema kwamba haelewi ni kwanini Seneta Linturi amekamatwa kwa haraka ilhali Mkurugenzi wa Mashtaka Umma DPP Nurdin Hajj aliagiza Idara ya Upelelezi kufanya uchunguzi kisha kuwasilisha ripoti yake tarehe 14 Mwezi huu ili kuamua iwapo Linturi angechukuliwa hatua za kisheria.
Haya yanajiri huku Baadhi ya wandani wa naibu wa rais William Ruto kusema kwamba Serikali inafanya ubaguzi wa kisheria kwa kuwanyanyasa. Hii ni baada ya kukamatwa kwa seneta Linturi kufuatia matamshi ambayo yamedaiwa kuwa ya uchochezi.
Kwa upande wake Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga na mwenzake wa WIPER Kalonzo Musyoka pamoja na Musalia Mudavadi wa ANC wakiwa tayari wamekosoa kauli hiyo.