HabariNewsSiasa

Mratibu wa utawala wa bonde la Ufa George Natembeya amejiuzulu.

Mratibu wa utawala wa bonde la Ufa George Natembeya
amejiuzulu. Natembeya amejiuzulu kufuatia lengo lake la kujitosa katika
masuala ya siasa kwani anakimezea mate kiti cha ugavana katika
kaunti ya Trans Nzoia. Katika kikao na waandishi wa habari, Natembeya amemshukuru
rais Uhuru Kenyatta kwa ushirikiano wake katika kuhakikisha
kwamba usalama unaimarishwa. Vilevile amezishukuru idara mbalimbali za kiserikali hususan zile za
usalama kwa kushirikiana naye katika juhudi zake za kudumisha
amani eneo la bonde la ufa.