HabariNewsSiasa

WAKENYA KUWASILISHA MAONI YAO KUHUSU MSWADA TATA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA VYAMA VYA KISIASA KUANZIA HII LEO HADI JUMATANO WIKI IJAYO.

Bunge la seneti limewaalikaWakenya kuwasilisha maoni kuhusu
mswada tata wa marekebisho ya sheria ya vyama vya kisiasa wa
mwaka wa 2021 uliowasilishwa katika bunge la seneti siku ya
jumanne.
Hatua hii inajiri baada ya spika wa bunge hilo ken Lusaka kuagiza
kamati ya haki na sheria kuanzisha mchakato wa kukusanya maoni
kuhusu mswada huo huku karani wa bunge hilo Jeremiah Nyegenye
akiwataka wakenya kuwasilisha mapendekezo yao kuanzia hii leo
hadi jumatano wiki ijayo.
Wakenya walio na uzoefu wa mtandao wametakiwa kutuma maoni
yao kuhusu mswada huo kupita barua pepe ya
csenete@parliament.go.ke kisha kuambatanisha maoni yao kwenda
katika senateJLAC@gmail.com
Kamati ya haki na sheria bunge hilo bila shaka inayoongozwa na
seneta wa nyamira Okong’o Omugeni aidha itafanya kikao cha
kuchukua maoni bunge alamisi na ijumaa wiki kwanzia saatatu
asubuhi hadi saa kumi na moja jioni