HabariNews

Tume ya Huduma kwa Polisi NPS imetoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu miili iliyopatikana kwenye mto Yala.

Tume ya Huduma kwa Polisi NPS imetoa taarifa kwa vyombo vya habari ikisema kuwa kwa kipindi cha miaka miwili miili 19 imepatikana kwenye mto Yala kinyume na taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari kuwa miili hiyo ni ya matukio ya hivi karibuni.
Ili kuharakisha zoezi la miili kutambuliwa pamoja na uchunguzi wa kina kufanywa, msemaji wa polisi Bruno Shioso, amesema kwamba kikosi maalum cha makachero kutoka kwa idara ya upelelezi, kimetumwa katika eneo la mto Yala sawia na hospitali ya Yala level 4 ili kusaidia katika uchunguzi.
NPS vilevile imetoa wito kwa umma kuhusiana na yeyote mwenye taarifa ambayo itawasaidia katika uchunguzi kuiandikisha katika kituo chochote cha polisi kote nchini.