HabariNewsSiasa

WAKAAZI WA ENEO LA CHANGAMWE KATIKA KAUNTI YA MOMBASA WARAIWA KUJISAJILI KAMA WAPIGA KURA.

Wagombea wa nyadhfa mbalimbali za uongozi kupitia kwa chama cha ODM wameendeleza kampeni ya kuwarai Wakaazi wa eneo la Changamwe Kaunti ya Mombasa kujisajili kama wapiga kura, ili kuwaweka mamlakani viongozi waadilifu.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha ODM tawi la Kaunti ya Mombasa Mohammed Hamid Hamis, Wagombea hao wamewarai Wakaazi kulichukulia kwa uzito zoezi hilo.
Katibu wa chama hicho Kaunti ya Mombasa Geoffrey Busaka ameligusia swala la mchujo wa chama hicho, akisema ni wanachama watakaokuwa wamesajiliwa katika orodha ya chama hicho pekee ndio watakaoshiriki kura hizo za mchujo.

BY EDITORIAL DESK