Uncategorized

Watu 9 wafariki kwenye shambulizi katika eneo la Arabia kaunti ya Mandera.

Watu 9 wamethibitishwa kufariki na wengine kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kukanyaga bomu la kutegwa ardhini katika eneo la arabia kaunti ya mandera.
Idara ya polisi inasema kuwa shambulizi hili limetokea asubuhi hii leo huku majeruhi wakiendelea kupokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Mandera.
Tukio hili linajiri siku chache baada ya baadhi ya maboliz wa mataifa ya ughaibuni nchini kuwatahadharisha raia wake kuhusu shambulizi la kigaidi.