HabariNewsSiasa

Aliyekuwa afisa mkuu msimamizi katika wizara ya maswala ya kigeni Ababu Namwamba, sasa anawataka mawaziri wote wanaojihusisha na shughuli za siasa kujiuzulu kutoka serikalini.

Aliyekuwa afisa mkuu msimamizi katika wizara ya maswala ya kigeni Ababu Namwamba, sasa anawataka mawaziri wote wanaojihusisha na shughuli za siasa kujiuzulu kutoka serikalini.
Akizungumza wakati wa kujiondoa kwake kutoka serikalini kuanza kuhudumu kama msimamizi wa maswala ya uhusiano ya kimataifa ya kigeni katika afisi ya naibu wa rais William Ruto ,Ababu Namwamba amesema ni kinyume na sheria na maadili kuendelea kuhudumu serikalini ilhali unafanyia mgombea wa urais kampeni.