HabariMazingiraNews

Huenda kampuni za kupakia na kuuza maji kwenye chupa za plastiki zikajipata pabaya kutokana na shutma za uchafuzi wa mazingira.

Huenda kampuni za kupakia na kuuza maji kwenye chupa za plastiki zikajipata pabaya kutokana na shutma za uchafuzi wa mazingira.
Akiongea katika mahojiano ya kipekee na meza yetu ya habari, Mkurugenzi mkuu wa mamlka ya utunzaji mazingira NEMA kaunti ya Mombasa, Samuel Lopokoiyit, akizishtumu kampuni hizo kuwa mstari wa mbele katika kuchafua mazingira wanapofanya biashara zao nchini. Ameongeza kuwa mamlka hiyo iko kwenye mazungumzo kuweka sheria kali dhidi ya kampuni hizo ili kudhibiti utumiaji wa chupa za plastiki kwenye bidhaa zao. Wakati huohuo Lopokoiyit Amewaonya wakaazi wanaojihusisha na utupaji taka kiholela katika sehemu mbalimbali za kaunti hiyo akisema wanakwenda kinyume na sheria. Ameongeza kuwa mamlka ya NEMA inaendlea kuweka mazingira safi kaunti hiyo hasa katika sehemu makhsusi za utupaji taka akipigia mfano jaa Kubwa la Mombasa la zamani Kibarani lililohamishwa Mwakirunge.