HabariNewsTravel

Madereva wa masafa marefu kaunti ya Mombasa wanalalamikia msongamano mkubwa wa magari katika halmashauri ya Bandari pamoja na kituo cha kupima uzani wa matrela huko Mariakani wakimtaka Waziri wa uchukuzi James Macharia kuingilia kati suala hilo.

Kwa mujibu wa madereva hao inawachukuwa muda mrefu kuondoka katika sehemu hizo hususan wakati wa kuingia na kutoka bandarini mwa mji wa Mombasa.
Hata hivyo baadhi ya madereva hao wanadai kuwa masuala ya madereva kutoa hongo yameibuka tena hasa kwa wamiliki wa mizigo kutaka kushughulikiwa kwa haraka ili kuanza safari zao.
Aidha wameongeza kwamba kumekuwa na msongamano mkubwa nyakati za jioni katika kituo cha kupima uzani wa matrela huko Mariakani unaotatiza magari yanayosafiri kutoka Mombasa hadi Nairobi .