Uncategorized

Malkia Elizabeth wa Uingereza amekutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Malkia Elizabeth wa Uingereza amekutwa na maambukizi ya virusi vya corona.
Kasri la Buckingham limesema, Malkia ana dalili za kawaida kama za mafua.
Kasri hilo limesema kwamba kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 95 ataendelea kufanya shughuli zake nyepesi katika kipindi cha wiki chache zijazo na ataendelea kutibiwa na kufuata miongozo yote ya kupambana na maambukizi vya virusi vya corona.
Malkia Elizabeth tayari amepata chanjo tatu dhidi ya COVID.

>>newsdesk