AfyaHabariNews

WAHUDUMU WA AFYA KAUNTI YA MOMBASA NA TAITA TAVETA WATISHIA KUGOMA JUMA LIJALO.

Muungano wa madaktari, wauguzi, maafisa wa kliniki, wahuduma wa mahabara pamoja na maafisa wa huduma za dawa katika kaunti ya mombasa na taita taveta wametishia kugoma jama tatu juma lijayo iwapo serikali hizo zitadinda kuwalipa mishahara ya miezi 2 pamoja na malipo ya mikopo ya miezi 5.

Akizungumza na vyombo vya habari katika kaunti ya mombasa Mwenyekiti wa muungano wa madaktari KMPDU Dkt Mohammed Ahmed Mkuche amesema kuwa ifikikapo tarehe 6 hakuna huduma za afya zitakozoendelea katika kaunti hizo mbili.

Kadhalika Mkuche ameeleza kwamba tayari muungano huo umewasilisha kesi mahakamani kutafuta haki zao kwani kwa sasa hali ya maisha ya maafisa wa afya inazidi kudorora kila uchao.

Mwenyekiti huo aidha amesema kuwa licha ya kutuma notisi ya siku saba kwa mwajiri wao hakuna jibu lolote jambo ambalo wanadai kutokuwa imani nae.

Kauli yake imepigwa jeki na katibu wa muungano wa huduma za dawa kaunti ya mombasa.