AfyaHabariNews

Baadhi ya watahiniwa walazimika kufanya mtihani wa kitaifa hospitalini

Wasichana wawili wajawazito kutoka Msambweni ni miongoni mwa watahiniwa zaidi ya elfu 23 katika kaunti ya Kwale wanaofanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE wakiwa hospitalini.
Mkurugenzi wa elimu katika eneo bunge la Msambweni Abraham Nyamawi, anasema wasichana hao watalazimika kufanyia mtihani wao hospitalini baada ya kupata ujauzito.
Nyamawi amesema tayari msichana mmoja amepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Msambweni huku mwingine akiwa katika hospitali ya kibinafsi ya Kinondo Kwetu.
Kwa upande wake msaidizi wa kamishena katika eneo hilo Flavia Akumu amedokeza kwamba ngoma za usiku zimepigwa marufuku wakati huu wa mtihani.
Akumu amewataka wakaazi kutocheza disco nyakati za usiku ili kuhakikisha wanafunzi wanafanya mtihani huo katika mazingira mazuri.