HabariNews

Wanawake hapa nchini wanaungana na wenzao kuadhimisha siku ya kimataifa kuhusu wanawake.

Kongamano mbali mbali zinaendelea hapa Mombasa kusherehekea mafanikio na juhudi zilizopigwa na Mwanamke katika jamii.
Viongozi wa maswala ya wanawake kaunti ya Mombasa wanasema wanawake wamekuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo katika jamii.
Katibu mkuu wa chama cha United Green Movement Hamisa Zaja ametoa wito kwa viongozi wengi kuhakikisha mwanamke anapewa mazingira bora ya kutekeleza majukumu yake ikiwepo maswala ya uongozi.