HabariNews

Tume ya kitaifa huduma ya polisi nchini (national police service commission) imeanzisha zoezi la kutoa hamasa kuhusiana na usajili wa makurutu unaotarajiwa kufanyika 24 mwezi huu .

Tume ya kitaifa huduma ya polisi nchini (national police service commission) imeanzisha zoezi la kutoa hamasa kuhusiana na usajili wa makurutu unaotarajiwa kufanyika 24 mwezi huu .
Akiongea mjini Kwale baada ya kukutana na vijana katika eneo bunge la Matuga wakati wa kutoa hamasa hizo Naibu mkurugenzi wa tume hio Esther Mwatha amesema kuwa lengo kuu la hamasa hizo ni kuhakikisha vijana wanatambua vigezo vinanyohitajika wakati wa usajili huo.
Mwatha pia amewarai vijana kukoma kutumia mihadarati akisema kuwa vijana wengi wamekuwa wakifungiwa nje wakati vipimo vinapotoka huku wengi wakilalamikia kutengwa katika nafasi za ajira.
Ni kauli iliyoungwa mkono na kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Steve Oloo akisema vijana wengi wamekuwa wakisingizia kukosa ajira kila zoezi hilo linapofanyika bila kutambua makosa yao.
Akigusia swala la pesa Oloo amewataka vijana wote watakaohudhuria usajili huo kukoma kutoa hongo akisema kuwa usajili huo unafanyika bila malipo.