AfyaHabariLifestyleMakalaNews

Ukosefu Wa Malezi Bora wa tajwa kuwa Chanzo cha Ukosefu wa maadili miongoni mwa vijana.

Ukosefu wa malezi bora na kusahau mila na desturi zaki Afrika zimetajwa kuwa chanzo cha vijana na watoto wenye umri mdogo kukosa maadili mema na kujiunga na magenge ya uhalifu na hata kutumia mihadarati.
Kulingana na afisa mkuu wa maswala ya teknolojia Mahmoud Noor, amehoji kuwa chanzo kikuu kwa vijana hao kupotoka ni kutokana na malezi ya mzazi mmoja ambapo imechangia kwa familia hizo kukosa misingi ya kimaadili ya kuja pamoja kama familia kwa kuwaelekeza watoto wao jinsi ya kuwa na tabia njema kama ilivyokuwa ikifanyika hapo zamani.
Noor amewalaumu wazazi pia wakutotenga wakati maalum wakujumuika na watoto wao na kuongezea kuwa wazazi wengi pia wamejitosa kwenye suala zima la uraibu hali ambayo inakuwa ngumu kwa vijana au watoto hao kuondoka katika njia sawa kama inavyotaka jamii.
Hata hivyo Noor ameongezea kuwa ni wakati sasa kwa jamii kuwa na vituo vya mageuzi ya tabia kwa minajili ya kuwanasua watoto hao.
Wakati huo huo Noor amewasihi vijana kutoshiriki kwenye vurugu za kisiasa kwani huu ndio wakati mwafaka wanasiasa hutumia vijana hao kwa maslahi ya kuharibu amani kwa wananchi.