AfyaHabariLifestyleMombasaNewsScience

Wajane wakumbwa na changamoto za kujiendeleza kimaisha…

Viwewe vya wajane ni tatizo kubwa kwa waathiriwa kuweza kuendeleza maisha yao ya kawaida kama awali na kuendeleza jamii katika njia inayostahi hivyo ipo haja ya kukuza afya ya akili kwa wajane hao.
Ni kauli ya Mwanahamisi Bakari, mkurugenzi mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Akilimali hapa Pwani linalojihusisha na kuimarishaji wa wajane kisakolojia na kuwapa matumaini ya kuweza kuendelea kimaisha hata baada ya kufiliwa na waume zao akimtaja mwanamke kuwa kiungo muhimu katika jamii na endapo hatakuwa timamu basi watoto, familia, jamii na hata nchi kwa jumla huenda ikapoteza mwelekeo bora na tija ya Maisha.
Bakari ameyasema haya katika kongamano la mafunzo ya jinsi ya kupambana na hali tata wanazokumbana nazo wajane huko Tiwi kaunti ya Kwale akisema baada ya kufiliwa wajane wengi huachwa katika njia panda bila msaada au watu wa kuwajali hali inayowaathiri kiakili na kutatiza jamii nzima hivyo kama shirika wanajukumu la kurudisha tabasamu katika nyuso zao.
Kulingana na Asha Rashid mjane aliyeachiwa watoto watano miongoni mwao watatu wa mumewe ambao mama yao alikuwa keshafariki miaka mitatu kabla ya kifo cha mumewe anasema aliathirika kiasi kikubwa hangeweza kuzungumzia hali hiyo na kulishukuru shirika la Akilimali kwa kuhakikisha anarejea hali yake ya kawaida

>> news desk