HabariLifestyleMazingiraMombasaNews

Afueni kwa wahudumu wa uchukuzi wa hapa Mombasa.

Huenda ikawa ni afueni kwa wahudumu wa uchukuzi wa hapa Mombasa na hata ukanda wa Pwani baada ya mkurugenzi wa mamlaka ya kitaifa ya barabara KENHA katika ukanda wa Pwani Erick Wambua kutoa hakikisho kwamba wako tayari kukabiliana na vizingiti vyovyote ambavyo huathiri uchukuzi hususan katika msimu wa mvua unaotarajiwa hivi karibuni.
Wambua amesema kwamba watazipa kipaumbele barabara ambazo hufurika msimuwa mvua na kupelekea shughuli za uchukuzi kutatizika hapa Mombasa huku akieleza kuwa mamlaka hio pia itarekebisha nyufa ambazo hutokea barabarani panaposhuhudiwa mafurikao.
Vile vile Wambua ameeleza haja ya wahudumu katika sekta ya uchukuzi kutunza barabara akizitaja kama rasilimali muhimu katika kuendesha uchumi wa nchi.

>> News desk