HabariNews

Tume ya huduma za bunge PSC imewaorodhosha wawaniaji wa wadhifa wa karani wa bunge la kitaifakufanyika tarehe 11 mwezi Aprili mwaka huu.

Tume ya huduma za bunge PSC imewaorodhosha wawaniaji wa wadhifa wa karani wa bunge la kitaifa huku mchujo ukiratibiwa kufanyika tarehe 11 mwezi Aprili mwaka huu.
Katika taarifa PSC imewaorodhesha waniaji wanne kati ya 44 ambao waliwasilisha maombi.
Samuel Josephat Njoroge atakuwa wa kwanza kuhojiwa kuanzia saa nne hadi tano asubuhi, Mohammed Ali Mohammed akihojiwa kuanziwa saa tano unusu hadi saa sita sita unusu naye Eunice Wanjiku akihojiwa kuanzia saa nane mchana huku Serah Kioko akihojiwa kuanzia saa tisa unusu hadi saa kumi unusu.
Mahojiano hayo yatafanyika katika majengo ya bunge huku wawaniaji wakitakiwa kuwasilisha kitambulisho cha kitaifa, paspoti, vyeti vya masomo na vilevile stakabadhi za kuwaidhinisha kwa mchujo kutoka kwa idara ya upelelezi.