HabariMombasa

WAKAAZI WA ZIWA LA NG’OMBE WAITAKA SERIKALI YA KAUNTI YA MOMBASA KUTENGENEZA MABOMBA YA MAJI TAKA.

Wakazi wa ziwa la ngombe katika eneo bunge nyali kaunti ya Mombasa wanaitaka serikali ya kaunti ya kuwachimbia mabomba ya maji taka ili kuondoa mafuriko uya maji yanayoshuhudiwa kutokana na mvua mkubwa unaonyesha kwa sasa.
Katika mazungumzo na meza yetu ya habri wakazi hao wanadai kuwa tangia mvua kuanza kunyesha wameshindwa kuendeleza maisha kutokana na maji kuwepo kila mahali hali ambayo imepelekea hata huduma za hospitali kukosekana.
Aidha wanadai kuhofia afya zao kutokana na maradhi hatari yanayotokana na maji chafu.
Aidha mgombea wa kiti cha mca eneo hilo Mohammed Duba ametoa chanagamoto kwa viongozi walioko mamlakani kurekebisha hali hiyo haraka iwezekanavyo.

BY EDITORIAL DESK