HabariLifestyleMombasaNews

WAKAAZI WA ZIWA LA NG’OMBE WAZITAKA IDARA YA MAHAKAMA NA POLISI KUTOMWACHILIA MSHUKIWA ANAYEDAIWA KUWALAWITI WATOTO 8.

Wakazi wa eneo la mbuyuni, ziwa la ngombe eneo bunge la Nyali wameghadhabishwa na hatua ya jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 30 anayeshukiwa kuwalawiti watoto wakiume 8 walioko chini ya miaka 10 na kuitaka idara ya mahakama pamoja na idaara ya polisi kutomwachilia huru wakihofia maisha ya watoto wao.
Wakizungumza na meza yetu ya habari wenyeji hao waliojawa na majonzi wameeleza kuwa jamaa huyo amekuwa akiwadahaa watoto hao kwa kuwapa pesa na vitabu kisha kuwatendea unyama huo hatua wanayodai kuwa imewacha maisha ya vijana hao katika hali ya taaruki.
Aidha wamehapa kuchukua sheria mikononi mwao iwapo serikali itamwachilia huru mshukiwa huyo kwa dhamana.
Akidhibitisha kisa hicho mzee wa mtaa eneo hilo Khemedi Salim ametoa ilani kali kwa kila mmoja ambae anania kama hiyo akisema kuwa idara ya usalama iko imara kuhakisha kuwa wahalifu wanachukiliwa hatua kali za kisheria.