HabariMombasaNewsSiasa

FIDIA KWA WAVUVI.

Mzozo wa fidia kwa wavuvi katika kaunti ya Lamu uliodumu kwa miaka minne sasa umefika kikomo baada ya makubaliano kati ya serikali na wavuvi.
Kwenye kikao mjini Lamu, wavuvi hao kupitia wakili wao wamekubali ridhaa hiyo ya shilingi bilioni 1.76 ambayo ni asilimia 65 fidia iliyotolewa na Mahakama Kuu mwaka wa 2018.
Kamishena katika kaunti ya Lamu Irungu Macharia aliyeongoza kikao hicho, amesema malipo hayo yatafanyika kabla ya mwezi wa nane mwaka huu.
Mwenyekiti wa wavuvi hao Somo Mohamed Somo pamoja na baadhi ya wavuvi wameshabikia uamuzi huo ambao jumla ya wavuvi 4,734 watafidiwa.
Somo amesema kila mvuvi atapokea shilingi laki 241 huku wavuvi zaidi ya sitini wakiripotiwa kufariki.