HabariMazingiraNews

Wadau wa Mazingira Mombasa waanzisha kampeni kuhamasisha wanafunzi katika shule za umma na zile za kibinafsi kuhusu maswala ya kutunza mazingira.

Wadau katika sekta ya Mazingira kaunti ya Mombasa wameanzisha kampeni ya kuhamasisha wanafunzi katika shule za umma na zile za kibinafsi kuhusu maswala ya kutunza mazingira.
Katika kampeni hiyo wanafunzi hao wanashiriki upanzi wa miche ya aina mbali mbali ya miti Pamoja na kufanya usafi.
Mwingi Chokwe afisa wa shirika la mazingira la Clean Mombasa CBO, anasema hamasa hiyo kwa wanafunzi inamanufaa makubwa maishani mwao n ahata katika kizazi cha siku zijazo katika kulinda mazingira.
Chokwe vile vile amedokeza kuwa wanashirikiana na wavuvi katika mtaa wa mabanda wa Moroto kupanda miche ya Mikoko Pamoja na kusafisa mazingira ya bahari ili kurejesha hadhi ya ufuo wa bahari wnwo hilo.
Kampeni hiyo imezinduliwa katika shule za msingi za Kaa chonjo na bahari eneo la Tudor.

BY EDITORIAL DESK