HabariNewsSiasa

Mahakama yazuia kwa muda IEBC kumwidhinisha aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko kuwania ugavana Mombasa.

Mahakama kuu ya Mombasa imezuia kwa muda tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC dhidi ya kumwidhinisha aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko kuwania ugavana Mombasa.
Agizo la mahakama limetolewa siku chache baada ya mashirika matatu ya kijamii; Haki Yetu, Kituo cha Sheria na Transparency International kuwasilisha kesi mahakamani ya kumzuia Sonko kuwania ugavana.
Kwa sasa IEBC haitamruhusu Sonko kuwania ugavana Mombasa mpaka pale kesi iliyowasilishwa mahakamani dhidi yake itasikizwa na kuamuliwa.
Kesi hiyo itasikizwa 24/05/2022.

BY EDITORIAL DESK