HabariMazingiraNewsSiasa

Wakaazi wa kaunti ya Mombasa wanaendelea kuhanganika kutokana na huduma duni ambazo zimekuwa zikitolewa katika kaunti hiyo.

Mgombea huru wa wadhifa wa useneta Mombasa Mohammed Amir amesema wakaazi wa kaunti ya Mombasa wanaendelea kuhanganika kutokana na huduma duni ambazo zimekuwa zikitolewa katika kaunti hiyo.
Amir amesema kwa muda wa sasa wakaazi Mombasa wamekuwa wakihangaika kutafuta huduma bora za afya vile vile huduma za maji licha ya serikali ya kaunti kupokea mgao wa fedha kutoka serikali kuu.
Amir anadai seneta aliyemadarakani kwa sasa Mohammed Faki amekosa kuwawajibisha maafisa husika hali inayochangia mahangaiko hayo.