Chama cha wana famasia nchini kimepinga uteuzi wa Terry Ramadhani kama afisa mkuu wa mamlaka ya usambazaji dawa na vifaa vya matibabu almaarufu KEMSA.
Chama hicho kinasema kuwawadhifa huo unafaa kupewa mtu mwenye tajriba katika maswala ya uagizaji.
Wanasema kuwa uteuzi huo umekiuka sheria za KEMSA na kuwa Terry hana ujuzi kwenye maswala ya dawa na vifaa vya matibabu au uagizaji wa bidhaa hizo.
Aidha chama hicho kimedai kuwa Terry ni mmoja waliobuni mahitaji ya kazi hiyo kabla ya kujiuzulu kutoka kwenye bodi hiyo na kutuma maombi yakutafuta kazi ya afisaa mkuu wa KEMSA.
Wanafamasia sasa wanatishia kumtimua ofisini iwapo atakubali uteuzi huo.