HabariMombasaNewsSiasa

NAIBU WA RAIS AREJEA PWANI.

Naibu wa Rais ambaye pia ni mpeperushaji bendera wa muungano wa Kenya Kwanza William Ruto anatarajiwa kuanza ziara yake ya kampeni kwenye mkoa wa pwani hii leo.
Ruto anatarajiwa kuzuru kaunti ya Kilifi leo ambako atakaribishwa na gavana Amason Kingi na Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa licha ya kuweko kwa tofauti za kisiasa baina yao.
Ziara ya naibu wa Rais inakuja siku chache baada ya kinara wa ODM na mpeperushaji bendera wa Azimio la Umoja Raila Odinga kuzuru mkoa huo ili kujipigia debe.
Itakumbukwa kwamba pwani imekua ngome ya Raila Odinga ila umaarufu wa naibu wa rais unakuwa kwani hivi sasa ana magavana wa Kilifi Amason Kingi na wa Kwale Salim Mvurya kwenye mrengo wake.
Aidha, Ruto anatarajiwa kufanya mikutano kumi na mojaya hadhara na kuwa na majukwaa ya kiuchumi kwenye kaunti zote tano za Pwani.

>>news desk