Idara ya usalama Kwale inasema imeanzisha oparesheni ya kufunga maeneo yanayouzwa vileo kinyume na sheria.
Naibu kamishna eneo la Msambweni Lotiatia Kipkech anasema ni sharti wamiliki wa vilabu vya pombe wafuate sheria ili kuthibiti uuzaji wa pombe haramu zinazo hatarisha maisha ya wateja wao.
Lotiatia ameongeza kuwa anahofia sehemu hizo huenda zikatumika kama maficho ya wahalifu hususan msimu huu wa kampeni za uchaguzi mkuu.
Amesema hayo katika kikao cha kutafuta mikakati ya kuimarisha usalama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti 9.
>>news desk