AfyaHabari

Idara ya afya nchini imesema huenda kukashuhudiwa ongezeko la wagonjwa wa akili.

Idara ya afya nchini imesema huenda kukashuhudiwa ongezeko la wagonjwa wa akili nchini kutokana na hali ngumu ya maisha.
Daktari wa magonjwa ya akili katika hospitali ya rufaa ya King Fahd katika kaunti ya Lamu Grace Kinyanjui amesema ugonjwa wa akili wamesababisha madhara mengi kwa jamii yakiwemo mauaji.
Kinyanjui amesema licha ya ugonjwa wa akili kuwa na tiba, wengi wamekosa kutafuta tiba wakiuhusisha ugonjwa huo na imani potofu.
Amesema takwimu kutoka kwa wanasayansi zinaonyesha kwamba mtu mmoja kati ya watu wanne wanaougua ugonjwa huo ama wataugua ugonjwa huo siku zijazo.

>> News Desk…