AfyaHabari

Idara ya Afya kaunti ya Taita Taveta kuzindua mradi wa hamasisho la matibabu ya saratani.

Idara ya Afya kaunti ya Taita Taveta inasema inapanga kuzindua mradi wa hamasisho la matibabu ya saratani utakao wahusisha watu wanaoishi na ulemavu.
Mradi huo unalenga watu wenye ulemavu wa macho, kusikia na wahudumu wa kijamii wa afya wasio na ulemavu watakao jitolea kufanikisha mradi huo.
Afisa mkuu mtendaji wa huduma za afya kaunti hiyo John Mwakima amesema kaunti hiyo ni kati ya kaunti saba zilizoteuliwa kuendesha mradi huo kwani Taita Taveta imepiga hatua katika kutambua mapema namna ya kukabili saratani.
Mwakima amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano na shirika la Amref Health Afrika, Roche East Afrika na serikali ya kaunti ya Taita Taveta.

>> News Desk…