Jamii ya Waboni katika kijiji cha Mswakini kaunti ya Lamu wanalalamikia ukosefu wa huduma za matibabu, elimu, maji na usafiri, huku wakiitaka serikali ya kaunti na ile ya kitaifa pamoja na wahisani kuingilia kati swala hilo.
wakiongozwa ni Tima Boge wamesema licha ya kilio chao cha muda mrefu, wamekosa maji ya matumizi ya nyumbani na vile vile wamekosa dawa katika kituo cha afya kilichoko eneo hilo.
wamesema kunahaja ya kuongezwa kwa madaktari katika kituo hicho cha afya, ambacho kwa sasa kituo hicho kina daktari mmoja hali ambayo inatatiza kushughulikiwa kwa wagonjwa.
Wamesema akina mama wajawazito wametatizika wakati wanapopelekwa kituoni humo kujifungua, huku baadhi ya wagonjwa wakifariki wanapokosa kuhudumiwa kwa wakati.

>>News Desk