HabariKimataifa

Zaidi ya watoto 800 wamepoteza mawasiliano na familia zao.

Shirika la Msalaba Mwekundu limesema zaidi ya watoto 800 wamepoteza mawasiliano na familia zao kufuatia mapigano makali kati ya wanajeshi wa serikali na waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Afisa mawasiliano wa shirika hilo, Irene Nakasiita amenukuliwa na shirika la habari la Ufaransa AFP akisema kwamba watoto 716 wameorodheshwa nchini Uganda pekee, huku wengine 155 wakiwa wameunganishwa na familia zao.
Ghasia zilizozuka upya katika miezi michache iliyopita zimewalazimisha maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao katika eneo la Rutshuru karibu na mpaka wa Congo na Uganda.

>> News Desk…