Wakaazi eneo bunge la Ganze kaunti ya Kilifi sasa wanapendekeza kuwekwa kwa uwa ili kuzuia wanyama pori kutangamana na wakaazi eneo hilo.
Wakiongozwa na mbunge wa eneo hilo Teddy Mwambire wakaazi hao aidha wanazitaka serikali za kaunti ukanda wa pwani kushirikiana ili kuzuia hayawani hao ambao wanahatarisha maisha ya wanadamu kwa sasa.
Mwambire anasema endapo serikali haitasaidia huenda wakaazi ambao wengi wao wanategemea kilimo wakakosa chakula katika siku za usoni kwani hayawani hao sasa wanaharibu mimea yao.
Kauli ya mjumbe huyo imeungwa mkono na naibu chifu wa Ndigiria Samson Kahindi anayesema maisha wa wakaazi kwa sasa yako hatarini kufuatia uvamizi huo.
Amependekeza kuwa shirika la huduma kwa wanyama pori KWS kuwazuiya wanyama hao kutoka kwa mbuga ya wanyama pori ya Tsavo ili kulinda maisha ya wakaazi eneo hilo.
Wawili hao wameyasema hayo huku shirika hilo la wanyama pori tayari likituma ndege aina ya Helicopter ili kuwaregesha Ndovu waliokuwa wakizurura ovyo eneo hilo.
>> Editorial Desk…