Habari

Hakuna mpango wa kuuza bandari.

Waziri wa fedha Ukur Yattani amesema hakuna mpango wa kuuza bandari za humu nchini kwa kampuni ya Dubai Port World FZE.

Yattani amekana madai ya muungano wa kenya kwanza kwamba rais Uhuru Kenyatta na mpeperusha bendera wa azimio Raila Odinga wametia Saini Mkataba wa kuziuza bandari za Mombasa, lamu, Naivasha na Kisumu kwa kampuni hiyo.

Yattani badala yake mpango uliopo ni wa ushirikiano baina ya serikali na kampuni hiyo kwani itakuwa inasimamia shughuli za bandari wala sio za kuikabidhi kabisa, inavyodaiwa na kenya kwanza.

Kulingana na Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi katika muungano huo, Yattani akishirikiana na mwanasheria mkuu wa serikali Kihara Kariuki, ndio waliotia Saini hatua ya kuikabidhi kampuni hiyo usimamizi wote wa shughuli za bandari.

>> Editorial Desk…