Huduma za kampuni ya Modern Coast Express Limited zimesimamishwa kufuatia ajali mbaya iliyotokea hapo jana jioni na kupelekea vifo vya watu 34.
Kulingana na NTSA kwa sasa inaendelea na uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo unaendelea huku huduma za kampuni hiyo zikilemazwa kwa muda katika njia zake zote nchini.
Njia hizo ni pamoja na Nairobi-Mombasa, Nairobi-Thika-Embu-Meru-Maua, Mombasa-Makindu-Wote-Kitui-Machakos na njia za Nairobi-Narok-Kisii-Homa Bay-Migori-Isibania.
Hakuna basi lolote la kampuni hiyo ambalo litaruhusiwa barabarani kufuatia hatua hiyo.
Basi lililohusika kwenye ajali Jumapili Inaripotiwa kupoteza mwelekeo na kuacha barabara baada ya breki zake kushindwa kufanya kazi.
Basi hilo lilianguka umbali wa futi 40 hadi kwenye mto Nithi.
Majeruhi wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Chuka na Hospitali ya Misheni ya PCEA Chogoria.
BY EDITORIAL DESK