HabariNews

WAZAZI WANAOFELI KURIPOTI VISA VYA WATOTO WAO KUWA WAJAWAZITO WAONYWA KILIFI.

Onyo kali imetolewa wa wazazi wanaofeli kuripoti visa vya watoto waliochini ya umri wa miaka kumi na minane kuwa wajawazito kwamba hatua kali za sheria zitakabiliana nao.
Kaunti ya Kilifi ni miongoni mwa kaunti zinazoorodhesha visa vingi vya mimba za utotoni, kaunti hii ikirekodi takriban visa elfu saba mwaka 2021 haya ni kwa mujibu wa ripoti mwaka 2021 ya baraza la kitaifa la idadi na maendeleo ya watu NCPD.
Kulingana na mgombea huru wa uwakilishi wa kike kaunti hii ya Kilifi Mary Luvuno Kombe, visa hivyo vimeongezeka kutokana na kesi hizo kutatuliwa kwa wazee wa mitaa na njia za kinyumbani.
Ameeleza kuwa atakapofanikiwa kunyakuwa wadhifa huo, atahakikisha kuwa kesi hizo zinafikishwa kortini na kusimamiwa na ofisi yake mpaka zitakapotamatika.
Aidha ametoa onyo kali kwa wazazi wanaohujumu kesi kwa kupoteza ushahidi ama kukosa kufika mahakani na kupelekea kesi hizo kufifia kwamba mkono wa sheria utawakabili.
Amesistiza kuwa hatua zote za sheria zitafuatwa ili kuhakikisha kuwa mwathiriwa anapata haki yake.

BY ERICKSON KADZEHA.