Shirika la msalaba mwekundu nchini linasema takriban watu milioni 4 wanahitaji msaada wa dharura wa chakula kufuatia atahari za ukame unaokumba kaunti 23 kufikia sasa.
Shirika hilo limeongeza kuwa Watoto wadogo walio chini ya umri wa miaka mitano, 900,042 wanakabiliwa na changamoto ya utapia mlo katika kaunti hizo kwa kukosa chakula huku wakina mama waja wazito na wanaonyonyesha wapatao 134,000 wakihangaikia chakula.
Ukame huo ambao umesababishwa na ukosefu wa mvua kwa zaidi ya misimu mitatu sasa umechangia kuaga dunia zaidi ya mifugo milioni mbili kaunti za Tanariver, mandera, isiolo, Turkana, Narok, garisa miongoni mwa kaunti nyengine za wafugaji.
Katika baadhi ya ya kaunti hizo wakaazi wamelazimika kutembea kwa mwendo mrefu wakisaka maji huku kwenye kaunti nyingine wakenya wakikosa kupata angalau hata chakula kimoja kwa siku.
Dkt Asha Mohammed ni katibu mkuu wa shirika la msalaba mwekundu nchini
BY EDITORIAL TEAM.