AfyaHabariNews

Kaunti ya Mombasa imetajwa miongoni mwa kaunti 20 zilizo katika uwezekano mkubwa wa tisho la virusi vya ebola.

Kaunti ya Mombasa imetajwa miongoni mwa kaunti 20 zilizo katika uwezekano mkubwa wa tisho la virusi vya ebola vilivyozuka nchini Uganda.

Miongoni mwa kaunti hizo pia ni Nairobi, Busia, Nakuru na Kiambu.

Wakaazi katika maeneo hayo wamahimizwa kuripoti kisa chochote kisicho cha kawaida cha kiafya

Akitoa habari jinsi wizara ya afya imejiandaa kukabilina na virusi hivyo endapo vitaripotiwa humu nchini Mkurugenzi wa afya daktari Patrick Amoth amesema wameweka mipango ya kuwapima wanaoingia humu nchini kupitia kaunti zilizo mipakani.

Hapo nyuma mkurugenzi wa afya ya umma daktari Francis Kuria amaesema idara ya afya nchini imejiweka tayari kimatibabu iwapo kutatokea dharura yeyote ya home ya ebola nchini.

Katika kikao na wanahabari Daktari Kuria amesema maradhi ya Ebola wanaweza kuyadhibiti hivyo kuwatoa wasiwasi wananchi juu ya maradhi hayo.

Wadau hao wa afya wamehimiza mikakati zaidi kuwekwa na wahudumu wa afya kujitolea kupewa mafunzo zaidi na vifaa vya kinga.

BY EDITORIAL TEAM