HabariKimataifaNews

Helikopta mbili za Kijeshi Zagongana na kuwaua watu 10 nchini Malaysia

Watu kumi wamefariki dunia baada ya helikopta mbili za
jeshi la wanamaji kugongana angani wakati wa mazoezi
ya kijeshi ya gwaride la Wanamaji wa Kifalme Malaysia.

Helikopta mbili za kijeshi za Malaysia zimegongana na kuanguka
wakati zikifanya mazoezi angani mapema leo na kuwaua watu 10
waliokuwamo ndani yake.

Picha zilizosambaa mtandaoni zilionesha helikopta kadhaa zikiruka
usawa wa chini kwa mpangilio katika uwanja wa jeshi la
wanamaji, wakati zikifanya mazoezi kabla ya sherehe ya jeshi hilo
mwezi ujao.

Baadaye ndege hizo ziligongana na kuanguka na kusababisha vifo
vya watu 10.

Waziri Mkuu wa Malaysia, Anwar Ibrahim, ametuma salamu za
rambirambi kwa familia za wafiwa akisema kuwa taifa
linaomboleza msiba huo mkubwa.

Mwezi uliopita, helikopta moja ya walinzi wa pwani
ya Malaysia ilianguka kwenye mlango bahari wa Malacca.
Mwaka 2016, naibu waziri alikuwa miongoni mwa watu waliofariki
baada ya helikopta kuanguka katika jimbo la Sarawak nchini
Malaysia.

Na DW Swahili