HabariNews

Mshukiwa wa Ulanguzi wa Bangi ya Milioni 4 aachiliwa kwa dhamana ya shilingi 50,000

Mwanamke mmoja mtuhumiwa wa ulanguzi wa
mihadarati aliyekamatwa huko kaunti ya Kwale
amekanusha madai ya kupatikana na mihadarati.

Akiwa mbele ya mahakama mjini Kwale Regina Akoth Kungu
aliyekamatwa na misokoto ya bangi kilo 135 yenye thamani ya
shilingi milioni 4 amekana mashtaka dhidi yake.

Inaarifiwa kuwa mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 30
alikamatwa mnamo Jumamosi Aprili 21 nyumbani kwake eneo la
Diani akiwa na magunia kadhaa ya bangi na shilingi 12,100 pesa
taslim zinazoaminika kuwa kipato cha biashara hiyo haramu.

Idara ya Upelelezi DCI imesema mtuhumiwa huyo hata hivyo
ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 50,000 pesa taslim.
Kesi hiyo itatajwa juma lijalo Aprili 30 mwaka huu.

BY MJOMBA RASHID