Baadhi ya familia katika kaunti ya Tana River zinaendelea kuhangaika kutafta maji na chakula kufuatia makali ya ukame kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Wakaazi wanalazimika kutembea zaidi ya kilomita 24 kuteka maji ambayo wanauziwa shilingi 100 kwa kila lita 20.
Kwa mujibu wa mamlaka ya kitaifa ya kukabili ukame NDMA zaidi ya watu elfu 92 wanahitaji maji na chakula katika kaunti hiyo kufuatia kipindi kirefu cha kiangazi.
Mmojawapo wa Kijiji kilichoathiria zaidi ni Chifiri ambako baadhi ya Watoto wamesusia masomo.
Amina Onsino mkaazi wa eneo hilo anasema kuwa wafugaji pia wanahangaiika kuwatafutia mifugo wao malisho.
BY EDITORIAL TEAM