HabariNewsSiasa

GAVANA WA KILIFI GIDEON MUNG’ARO ATANGAZA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI.

Gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Mung’aro ametangaza baraza lake la mawaziri akitoa nafasi 4 kwa akina mama.

Akizungumza na wanahabari katika afisi yake Mung’aro amewafuta kazi mawaziri wote waliokuwa wakuhudumu katika hatamu ya mtangulizi wake Gavana Amason Kingi.

Amewataka mawaziri hao kufanya kazi kwa uadilifu endapo watapita msasa wa bunge la kaunti hiyo akiwaonya kuwa atakayezembea atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Wakati uohuo Gavana huyo amewataka mawaziri hao kutoa ushauri mwafaka kwa serikali hiyo sambamba na kufanya ukaguzi mara moja katika wizara zao katika kipindi kilichopita.

Majina hayo Kumi sasa yatawasilishwa katika bunge la kaunti hiyo wakati wowote kuanzia sasa ili wajumbe waweze kuyapiga msasa kabla ya kuyathibitisha.

BY EDITORIAL DESK