Bunge la 13 linapoanza vikao vyake rasmi hii leo, spika wa bunge la kitaifa Moses Masika Wetangula anakabiliwa na kibarua cha kutegua kitendawili cha ni mrengo upi ulio na wabunge wengi utakopata wadhafa wa kiongozi wa wengi katika bunge hilo.
Suala la kupatikana kwa kiongozi wa wengi limekumbwa na utata kutokana na mvutano baina ya mrengo wa azimio la umoja na mrengo wa serikali wa kenya kwanza, kila mmoja akidai kuwa na wingi wa wabunge ambapo tayari Mrengo wa Kenya Kwanza ulimteua Kimani Ichungwa kuwa kiongozi wake wa wengi huku mrengo wa azimio ukimteua Opiyo Wandayi Kuwa kiongozi wa wengi katika bunge hilo.
Ikumbukwe kwamba baadhi ya wabunmge wa azimio walijiunga na kenya kwanza jambo ambalo limeongeza idadi ya wabunge hao hatua ambayo viongozi wa azimio waliikashifu huku wakiitaja kuwa kinyume na makubaliano ya mkataba uliotiwa sahihi na viongozi wa vyama tanzu vya muungano huo.
Suala la hilo linakuwa na umuhimu kwa bunge kwani kamati mbalimbali za bunge hilo huundwa kwa kuzingatiwa upande wa wengi na wachache, wetangula akiwa na jukumu la kuhakikisha shughuli za bunge hazitaathirika kutokana na uamuzi atakaoutoa kuhusu ni mrengo upi ulio na wengi na ni upi wa wachache.
BY EDITORIAL TEAM