AfyaHabariNews

SERIKALI YA KAUNTI YA KILIFI YASEMA IMEWEKA MIKAKATI YAKUTOSHA ILI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KAUNTI HIYO.

Serikali ya kaunti ya Kilifi inasema kuwa imeweka mikakati yakutosha ili kuboresha huduma za afya ikiwemo kuongeza idadi ya wadi za wagonjwa katika hospitali kuu ya mji wa Malindi.

Kulingana na gavana wa kaunti hii Gedion Mung’aro , hatua hizo zitaanza kutekelezwa kuanzia juma lijalo kupitia ufadhili wa kampuni tofauti ili kutatua changamoto za maswala ya afya.

Akizungumza na wanahabari baada ya kuhutubia kikao cha kwanza cha bunge la tatu la kaunti hii, Mung’aro amedokeza kuwa serikali yake inalenga kuyaangazia kwa upesi maswala ya afya, kilimo, barabara miongoni mwa mengineyo.

Kauli hiyo imeungwa mkono na mwakilishi wa wadi ya Shella mjini humo Twaher Abdhulkarim, huku akidai kuwa serikali ya kaunti hii ina mipango kambe ya kuboresha utoaji wa huduma za afya.

Hata hivyo Twaher amebainisha kuwa juhudi za gavana wa kaunti hii zitafanikiwa kupitia ushirikiano wa bunge la kaunti hii.

BY EDITORIAL TEAM