HabariNews

Tabianchi ndani ya kaunti ya Kwale yapelekea wasichana wengi kunyanyaswa kimapenzi.

Umbali na ukosefu wa maji ya kutosha kufuatia mabadiliko ya tabianchi ndani ya kaunti ya Kwale umepelekea wasichana wengi katika eneo hilo kunyanyaswa kimapenzi.

Kwa mujibu wa afisaa kutoka shirika la kijamii la Crawn Trust Cindy Kobei amedokeza kuwa kiangazi kikali kinachoshuhudiwa katika baadhi ya sehemu hapa kaunti ya Kwale hususan sehemu kame kama eneo bunge la kinango na lungalunga kimesababisha mabwawa mengi kukauka hali inayowalazimu wasichana na pia wamama kutembea mwendo mrefu kutafuta maji hayo.

Aidha Kobei ameendelea kusema kuwa kutokana na hali hiyo ya ukame ambapo hakuna chakula wasichana wa sehemu hizo wameonekana kujiingiza katika ngono biashara katika fuo za bahari ili kuweza kujikimu kimaisha jambo alilolitaja kuwa miongoni mwa athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Wakati uo huo Kobei amesema kuwa shirika hilo ambalo linatathmini mabadiliko ya tabia ya nchi litatekeleza mradi wa kuhamasisha jamii kuhusuana na mabadiliko ya tabia ya katika kaunti nchini kwale ikiwa mojawapo.

Hata hivyo shirika hilo limeitaka serikali ya kaunti ya Kwale kubuni sheria zitakazo kabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na mengineyo.