HabariNews

Wakaazi wa Mwembeni katika eneo la Samburu kaunti ya Kwale walioachwa bila makao wanaomba msaada wa chakula.

Wakaazi wa Mwembeni katika eneo la Samburu kaunti ya Kwale walioachwa bila makao baada ya nyumba zao kuchomwa na watu wasiojulikana wiki iliyopita wanaomba msaada wa chakula kutoka kwa serikali.

Wakiongozwa na Mkala Mdoe, wakaazi hao wanadai kuwa kwa sasa wanakabiliwa na baa la njaa kufuatia ukosefu wa chakula.

Kulingana nao, watoto wa shule wameathirika zaidi kutokana na hali ngumu ya maisha inayowakumba baada ya mali yao kuteketea katika uvamizi huo.

Wakati uo huo, wakaazi hao pia wameitaka serikali kuwapatia usalama wa kutosha kwani wanahofia kuwa huenda wakavamiwa tena.

Wamesisitiza kuwa hawataondoka katika eneo hilo linalokumbwa na mzozo wa umiliki wa ardhi baina yao na bwenyenye mmoja.

BY EDITORIAL TEAM.