HabariNews

WAZIRI MTEULE WA UCHUKUZI KIPCHUMBA MURKOMEN AHOJIWA.

Kwa zaidi ya miaka 50 ya uhuru wa taifa la Kenya, barabara ambazo ni muhimu kwa kitega uchumi hazijapewa kipau mbele huku baadhi ya maeneo yakisalia na barabara mbovu.

Akizungumza mbele ya kamati ya bunge mapema hii leo waziri mteule wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen amesema kuna haja ya mgao sawa wa ujenzi wa barabara kote nchini.

Murkomen ameendelea kusema kwamba, makampuni yanayopewa zabuni za ujenzi wa barabara yanaishia kupata faida kubwa kutoka nchini na kuomba kandarasi hizo zipewe wakenya wenye uwezo ili usambazaji wa fedha utumike nchini na kukuza uchumi wa nyumbani badala ya mataifa ya kigeni.

Murkomen aidha amependekeza kuondolewa kwa maafisa wa trafiki na badala yake kutundikwa kwa camera za CCTV kuwakabili wanaovunja sheria za trafiki.

Kuhusu kurejesha nidhamu miongoni mwa wahudumu wa magari na bodaboda, Murkomen amesisitiza kuwa kuna swala la kutumika kwa teknolojia kuwakabili madereva wanaokiuka sheria huku akiahidi kuwakabili waharibifu wa barabara wanaong’oa vyuma ili kuviuza.

BY EDITORIAL DESK