Mashirika ya kijamiii yamesisitiza haja ya raisi William Ruto kuweka mikakati thabiti ya kuwachukulia hatua wale afisa polisi wote waliohusika na mauaji ya watu kiholela.
Mashirika hayo yamesisitiza kuwa yako imara kuhakikisha kuwa kila familia zilizoathirika na mauaji hayo watapata haki kisheria.
Katika mazungumzo na vyombo vya habari hapa mjini Mombasa, mashirika hayo yakiongozwa na Haki Afrika, MUHURI na Haki Yetu wamesema kwamba baada ya raisi Wilim Ruto kuthibitisha visa hivyo sasa wanamtaka kuwachulia hatua wale wote waliohusika katika mauaji hayo.
Vile vIle changamoto imetolewa kwa mkurugenzi mpya wa DCI Mohamed amir kulivalia njuga swala hilo sawa na kuhakikisha matukio kama hayo hayatashuhudiwa tena nchini.
Haya yanajiri siku chache tu baada ya rais kufutilia mbali kikosi maalum cha polisi, Special Service Unit ambacho alidai kilihusika pakubwa katika mauajoi ya wanachi.
BY EDITORIAL DESK