HabariNews

Kamanda wa polisi wa Msambweni Francis Gashoki amewaonya wakaazi wa eneo hilo dhidi ya kuingiza siasa katika suala la utafiti wa madini.

Kamanda wa polisi wa Msambweni Francis Gashoki amewaonya wakaazi wa eneo hilo dhidi ya kuingiza siasa katika suala la utafiti wa madini unaofanywa na kampuni ya Base Titanium.

Akizungumza katika eneo hilo, Gashoki amekana madai kuwa kampuni hiyo inawashurutisha wakaazi kufanyiwa utafiti wa madini katika mashamba yao.

Kamanda huyo amewataka wakaazi wanaopinga utafiti huo kutoingiza siasa ili kuzuia mgogoro wa ardhi baina ya wenyeji na kampuni hiyo.

Wakati uo huo, Gashoki amedai kuwa baadhi ya wakaazi wanaopinga utafiti wa madini hawana stakabadhi za umiliki wa ardhi zao.

Haya yanajiri kufuatia malalamishi ya baadhi ya wakaazi wanaopinga utafiti wa madini katika ardhi zao.

BY EDITORIAL DESK