HabariNews

Wakulima kaunti ya Kwale watakiwa kuyatayarisha mashamba yao.

Naibu kamishna wa Matuga kaunti ya Kwale Lucy Ndemo amewataka wakulima kutayarisha mashamba yao kwa ajili ya msimu wa mvua za vuli.

Akizungumza na wanahabari mjini Kwale, Ndemo amewahimiza wakulima katika eneo hilo kupanda mimea yenye uwezo wa kustahimili msimu huo.

Naibu huyo wa kamishna amesema kwamba hatua hiyo inalenga kutatua changamoto zinazowakumba wakulima wakati wa msimu wa mvua chache.

Wakati uo huo, Ndemo amewataka wakaazi kaunti hiyo kupanda miti kwa wingi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Afisa huyo tawala pia amesisitiza haja ya wakaazi kuitunza miti hiyo ili kutatua changamoto ya ukame inayoshuhudiwa kaunti hiyo.

BY EDITORIAL DESK